Mwanafunzi ajifungulia njiani wilayani Rombo
WATCH HERE
Mwanafunzi ajifungulia njiani wilayani Rombo
Mkuu wa wilaya ya Rombo, Limbris Kipuyo,
Mwanafunzi Mmoja wa shule ya sekondari yaTarakea wilayani Rombo Mkoani Kilimanjaro amajeifungulia njiani wakati akielekea hospitali huku wengine wa vidato tofauti wakibainika kuwa na ujauzito baada kufanyika kwa zoezi la upimaji shuleni hapo.
Akizungumzia suala hilo mbele ya Mkuu wa wilaya na waandishi wa Habari, Afisa taaluma wa wilaya hiyo Viane Mgoma amesema mwanafunzi aliejifungua ni wa kidato cha sita na alikua akijisikia maumivu ya kichwa.
Mgoma amesema kuwa suala hilo ni aibu kwa wilaya hiyo na halitavumuliwa hata kidogo huku akiongeza kuwa kuna usiri mkubwa kwa baadhi ya wazazi kuwaficha watoto wao wenye ujauzito ambao huwa wanawaficha majumbani kwao huku wakiwa na taarifa ya matatizo yao.
Afisa taaluma huyo ameongeza kuwa kwa mwaka 2015 wamepokea kesi 29 za wanafunzi waliopata ujauzito ambapo amesema ingawa ni asilimia ndogo sana ya wanafunzi wote lakini jambo hilo linapaswa kuchukuliwa hatua.
Akizungumzia vitendo vya ujauzito katika shule hiyo Mkuu wa wilaya ya Rombo, Limbris Kipuyo, amesema jambo hilo limechangiwa na baadhi ya walimu kufanya kazi kwa mazoea kwa kuacha kuwapima wanafunzi ujauzito mara kwa mara.
Mpaka sasa wanafunzi wa nne wakiwemo wawili wa kidato cha nne, Mmoja kutoka kidato cha tano, na mmoja kutoka kidato cha tatu wamebainika kuwa na ujauzito.

0 comments:
Post a Comment