Amber Lulu Aweka Wazi List ya Mastaa Aliotoka Nao Kimapenzi, ‘Aslay Kiboko Kabisa’


SeeBait

Amber Lulu Aweka Wazi List ya Mastaa Aliotoka Nao Kimapenzi, ‘Aslay Kiboko Kabisa’

Sio kawaida sana kwa mastaa wa bongo kufanya hivi, Msanii Amber Lulu ametaja orodha ya mastaa ambao amewahi kutoka nao kimapenzi.

Muimbaji huyo anayetikisa na ngoma ‘Jini Kisirani’ katika orodha hiyo amejikuta akimsifia zaidi Aslay kuliko hao wengine.

“Barnaba, Aslay, Rammy Galis naYoung Dee lakini Young Dee sio sana, hao wanatosha, hao wengine hapana,” amesema.

“Aslay nilishatoka naye ila alikuwa ni mtu fulani muelewa, yuko poa, ana heshimu mwanamke. Yuko noma, yuko vizuri, Aslay kiboko kabisa,” Amber Lulu ameiambia Clouds TV.

Katika hatua nyingine Amber Lulu amesema kuwa mpenzi wake wa sasa, Prezzo amechukia sana kufuatia kuvuja kwa video yake chafu akiwa na msanii Nuh Mziwanda, hata hivyo Amber Lulu amekanusha kuwa na mahusiano na Nuh Mziwanda.


SHARE

Author

Hi, Its me Hafeez. A webdesigner, blogspot developer and UI/UX Designer. I am a certified Themeforest top Author and Front-End Developer. I'am business speaker, marketer, Blogger and Javascript Programmer.

  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment