BREAKING: Taarifa kuhusu kutoonekana kwa Mwanafunzi Abdul Nondo|Tanzania Students Network Programme Public Notice

Miongoni mwa stori kubwa Leo March 7, 2018 ni kuhusu taarifa za kutoonekana kwa Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi Tanzania, Abdul Nondo ambae pia ni Mwanafunzi wa Chuo Kikuu Dar es Salaam ambaye ilidaiwa kapotea katika mazingira ya kutatanisha jana usiku majira ya saa 5 hadi 6 na kuacha ujumbe usemao “I AM AT HIGH RISK”

Akizungumza na AyoTV na millardayo.com Mkurugenzi wa idara ya Sheria ya Mtandao wa Wanafunzi Tanzania Paul Kisabo amesema  kwamba Abdul Nondo amepatikana mkoani Iringa katika wilaya ya Mafinga. 

Nanukuu “Nondo amepatikana yupo mafinga kituo cha polisi muda huu. Amezinduka jioni ya leo akiwa ametupwa, akauliza watu kwamba yuko wapi wakamwambia yupo mafinga. Akajivuta kwenda kituo cha polisi,” –

“Bahati nzuri alikuwa anakumbuka namba moja tu ya dada yake akaomba simu polisi na kumpigia dada yake, Dada yake pia akamjulisha baba yake mdogo wa huku dar tuliyekuwa nae leo” -Paul Kisabo

“Then kupitia namba ya polisi kituo cha polisi Mafinga Nondo ameongea na baba yake mdogo tuliyekuwa nae leo kupitia simu ya afande. Amenyang’anywa laini zake za simu ila simu yake anayo. Ila yupo salama.”-Paul Kisabo

Bonyeza PLAY hapa chini kumsikiliza Afisa Habari wa Mtandao wa Wanafunzi Tanzania

 

BREAKING: TAARIFA KUHUSU KUTOONEKANA KWA MWANAFUNZI ABDUL NONDO


SHARE

Author

Hi, Its me Hafeez. A webdesigner, blogspot developer and UI/UX Designer. I am a certified Themeforest top Author and Front-End Developer. I'am business speaker, marketer, Blogger and Javascript Programmer.

  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
  • Image
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment